Athari za kuamini majina na sifa zake Allah kwa mja
[سجل معنا ليظهر الرابط. ]1-kuabudu Kwa majiNa Na sifa zake Allah, kWaNi mja akiyajua haya majiNa huyaamiNi Kama atakavyo Allah Mtukufu, Na kuyafahamu maaNa yake ambayo yaNamuongezea imaNi yake Kwa Allah Mola Wake, ndio Allah aNatukuzWa Na kuadhimiWa kWa moyo uliomfahamu kWahiyo, mwenye kumfahamu Allah zaidi humuogopa zaidi’
2-kuongezeka Kwa ImaNi: Kuyatambua majiNa ya Allah mazuri Na sifa zake za juu, kuNamfanya mja ahisi ukubWa Wa Allah Mtukufu, jambo ambalo liNamuongezea muumin imaNi juu ya imaNi, Na unyenyekevu juu ya unyenyekevu Kwa Allah Mtukufu. {Na Wale WaNaokubali kuongoka aNaWazidishia uongofu Na aNaWapa (jaza) ya ucha mungu Wao.} (Muhammad: 17)
3-kumkumbuka Allah Na kumtaja : Mwenye kumjua Allah, humpenda, Na mwenyekumpenda mola Wake basi hukithirisha kumkumbuka Na kumtaja, kWasababu ameumiliki moyo Wake kWa kumpenda, mpaka akaWa hapendi ila aNachokipenda yeye, Wala hachukii ila aNachochukia yeye.
4-kumpenda Allah Mwenye nguvu Na utukufu: amesema Allah Mtukufu: {Na katika Watu Wapo WaNao chukua Waungu Wasio kuWa Mwenyezi Mungu. WaNaWapenda Kama kumpenda Mwenyezi Mungu. LakiNi Walio amiNi WaNampenda Mwenyezi Mungu zaidi Sana.} (AL baqarah: 165)
Atakapojua mja ukubWa Wa sifa za Mola Wake Na utukufu Wake Nafsi yake, basi Nafsi yake huzama Na kuelekea kWaMola Wake, Na hufungamaNa Naye Allah aliye takasika, Nafsi yake ikaWa Na raha Na Mola Wake kWasababu ya ukamilifu Wa utukufu Wake Na uzuri Wake, ndio akaWa mWaNadamu aNapata raha kWa maneno ya Mola Wake, Na aNajiliWaza kWa kumuomba Na kumtarajia yeye Na kumkhofu, kWasababu mapenzi ya Allah Mtukufu yaNaelekeza kWa haya, utampata mja aNampenda Allah Na aNampenda aNaye mpenda Allah.